HomeResourcesSabbath School quarterly

Jifunze zaidi

05/06/2026

Biblia mara nyingi hutumia sitiari za kilimo kuelezea hali yetu ya kiroho. Hosea 10:12 ni mfano mmoja unaoshika kwa uzuri yale tuliyojadili juma hili;

Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.

Tunapanda, tunavuna, tunalima udongo mgumu, na kumtafuta Mungu aje karibu nasi. Udongo mgumu wa mioyo yetu lazima utayarishwe na kuwa tayari kwa mvua (Roho Mtakatifu) kuunyeshea. Mungu anaweza kutupa shauku ya kuandaa udongo, lakini mwishowe, uhusiano pamoja Naye ni wa ubia (tazama Wafilipi 2:12, 13). Tunapaswa kumgeukia, kumwendea, na kushikamana naye. Kisha Yeye hufanya kazi ndani yetu kutimiza yote yaliyosalia.

Mfano mmoja mzuri wa kushikamana na Mungu unaweza kupatikana katika aya hizi: “Macho yenu yameona aliyoyatenda Bwana kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, Bwana, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako. Bali ninyi mlioambatana na Bwana, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo” (Kumbukumbu la Torati 4:3, 4).

Masawali ya Kujadili

Muhtasari: Kutambua dhambi zetu kwa kuitikia msukumo wa Roho Mtakatifu na kujisalimisha kwa toba ni sehemu muhimu ya kuwa na uhusiano unaostawi na Mungu. Kujua kwamba tumesamehewa kabisa na kufunikwa kwa vazi la haki ya Yesu ni uzoefu wa kubadilisha maisha kwa kiwango cha juu kabisa kwa mwanadamu. Si tu kwamba tunahisi mzigo wa dhambi umeondolewa, bali tunahisi upendo wa Mungu ukituzunguka tunapovutwa karibu zaidi na Yeye. Hili hutufunga na Mungu, hutuimarisha kiroho, na hutuvuta kumpenda kwa kila sehemu ya nafsi yetu.