HomeResourcesSabbath School quarterly
Mungu ni Mtakatifu
06/04/2026
Utakatifu si neno linalotumiwa na watu mara kwa mara kwenye lugha yao kila siku, pengine kwa sababu vipo vitu vichache sana vitakatifu vinavyotuzunguka. Sabato ni siku takatifu katika wakati, na Mungu kwa kweli, ni mtakatifu. Lakini maisha yetu ya kila siku yana upungufu wa utakatifu.
Ukifanya uchunguzi wa sifa zinazohusiana mara kwa mara na tabia ya Mungu, utagundua kwamba utakatifu ni kiini cha namna Mungu alivyo. Lakini hilo linamaanisha nini?
Biblia inapomwelezea Mungu kama kielelezo cha juu cha utakatifu, ina maana kwamba Yeye ni mtupu kabisa wa uovu na amejitenga kabisa na uovu na dhambi, Mungu ni mwema kwa asilimia 100 mwanzo hadi mwisho. Kwa maana hii, utakatifu wa Mungu ndiyo msingi wa sifa Zake nyingine zote.
Kwa mfano, upendo wa Mungu ni upendo safi, mtakatifu—upendo usio na ubinafsi wowote na nia za kujisifu. Ujuzi Wake (kujua yote) ni ujuzi mtakatifu, ukimaanisha kuwa hauna nia mbaya. Je, ungemwamini Mungu ajuaye yote kama asingekuwa mtakatifu? Badala yake, tungemwogopa, na jambo ambalo lenyewe ni sahihi kabisa.
Uweza wa Mungu (kuwa mwenye uwezo wote) ni uweza mtakatifu. Hebu fikiria Mungu ambaye ni mweza wa yote lakini si mtakatifu. Anaweza kuwa dhalimu mwenye nguvu, mwovu. Utakatifu wa Mungu pekee unaturuhusu na kutuwezesha kumpenda kweli, kwa sababu Yeye ni mwema tangu mwanzo hadi mwisho. Hii ndiyo sababu utakatifu labda ndiyo sifa muhimu zaidi kuelewa kuhusu tabia ya Mungu. Walakini, labda, ni mojawapo isiyoeleweka pia.
Fikiria watu wanaotajwa katika Biblia kama vile Musa, Isaya, Ezekieli, Danieli na Yohana, walikuja mbele za Mungu. Mwitiko wao wa kwanza ulikuwa upi? Walivua viatu vyao, wakaficha nyuso zao, au wakaanguka chini kana kwamba wamekufa. Kama wanadamu, sisi ni wenye dhambi na waovu kiasi kwamba hatuwezi kuthubutu kusimama katika kuwepo kwa Mungu. Mwanadamu yeyote anayeutazama uso wa Mungu hataishi. Vivyo hivyo, wakati Ellen G. White alipoingia kwenye maono, mara kwa mara alilia, "Utukufu... Utukufu.... Utukufu,” kwani ndilo neno pekee lililoonekana kuelezea kile mengi kati ya yale aliyoyaona. Na kwa kweli, viumbe walio hai wanne hawakomi mchana na usiku katika kusema “ 'Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!’ ” (Ufu. 4:3)