HomeResourcesSabbath School quarterly

Upendo wa Milele

31/03/2026

Baada va kuonesha hali yetu ya kutojali, Yesu anatuambia kwamba hili ni jambo ambalo yapasa kulishinda. “ ‘Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi' ” (Ufu. 3:21). Kwa baadhi yetu, inaweza kuwa vita kuu zaidi ambayo tumewahi kukumbana nayo—kwa kutambua tu hali yetu dhaifu, ya kujitosheleza; kukubali kemeo la Yesu; kutubu; na kupokea vazi la Yesu la haki juu yetu kwa macho ambayo yanaona hakika.

Kinachoshangaza sana ni kwamba Yesu anaelewa hali yetu ya kutojali, ya uvuguvugu na anajihusianisha nasi (si kwamba Yesu aliwahi kuwa vuguvugu wakati wowote). Anasema, “ 'Kwake yeye ashindaye ... kama mimi nilivyoshinda' ” (Ufu. 3:21). Kwa sababu Yesu alikufa ili kutuokoa, ameshinda dhambi na adhabu yake. Yeye anaelewa vita vya dhambi ambavyo tunakabiliana navyo na anaahidi kutusaidia.

Watu wengi kwenye Biblia waliitikia mwaliko wa Mungu wa kuwa kwenye uhusiano wa agano pamoja na Yeye. Hizi ndizo simulizi au mada kuu ya Biblia nzima. Tunapowatazama baadhi ya watu hawa, tunaweza kuona kwamba Mungu alishirikiana nao kwa njia tofauti kwa nyakati tofauti.

Simulizi hizi zinatufundisha nini kuhusu jinsi Mungu anavyoshughulika na watu katika hali mbalimbali?

Iwe Mungu alitembea kimwili au uhalisi na watoto Wake au kama Alizungumza nao tu, ukweli ni kwamba daima Ametamani kuwa karibu na wanadamu. Haidhuru uhusiano wako na Mungu uwe vipi leo, Mungu anataka kuwa karibu nawe. Tunaweza kusoma kuhusu wazo hili katika Yeremia 31:3, 4 hapa chini:

“BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele; kwa hiyo nimekuvuta kwa fadhili zangu; mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa.”

Iwe siku yako inaanza au inaisha sasa hivi, Mungu anakutafuta na kukusubiri, akitaka kukusogeza karibu naye. Anataka kujenga—au kujenga upya—uhusiano wako Naye. Kama hilo halitokei, kosa liko upande wako, si Wake.