HomeResourcesSabbath School quarterly
Kaa
01/04/2026
Wanafunzi walimfuata Yesu chini ya ngazi nyembamba kutoka chumba cha juu hadi barabata iliyo chini. Walipokuwa wakitembea pamoja hadi Gethsemane, katika ule uliokuwa usiku wa maana sana katika historia ya dunia, pengine hawakutambua jinsi baadhi ya maneno ya mwisho ya Yesu kwao katika Chumba cha Juu yalivyokuwa yenye kutia uchungu kweli.
Maneno haya, yaliyosemwa na Yesu Mwenyewe, yanaelezea jinsi uhusiano wa karibu na Mungu ulivyo. Angalia neno linalorudiwa, si mara mbili tu bali mara 10: kaa. Kukaa ndani ya Yesu ni kuishi katika uhusiano Naye.
Anapoukabili Msalaba, Yesu si tu kwamba anasisitiza umuhimu mkubwa wa kukaa huku ndani Yake, lakini Anasema kwa uwazi na kwa urahisi kipengele cha uhalisi wa jinsi inavyoonekana maishani mwetu.
Ambayo ni: Yesu ni mzabibu, sisi ni matawi. Kama matokeo ya kukaa (kuunganishwa) Naye, matunda yatakua kwenye matawi yetu. Sisi wenyewe hatuwezi kufanya matunda yakue. Wakati mwingine tunaweza kuonekana kana kwamba tunadumu, lakini ushahidi utakuwa katika ukosefu wetu wa matunda, na hatimaye matawi yetu yatakauka. Ikiwa tumekauka, Mkulima wa Mizabibu hatimaye atakata matawi. Bila kujali tunazaa matunda au la, matawi yetu yatapogolewa.
Wakati huo huo, sisi sote tunakabiliana na changamoto na nyakati zenye maumivu. Tukikaa ndani Yake, nyakati hizi zitazaa matunda zaidi kwa muda mrefu. Kuzaa matunda kunathibitisha sisi ni nani (wanafunzi). Tunazaa matunda ili kumletea utukufu (si kwetu wenyewe). Kukaa ndani ya Yesu kunamaanisha kushika amri Zake, ambazo ni onesho la tabia Yake nzuri ya upendo usio na ubinafsi. Kukaa ndani ya Yesu huleta furaha kuu. Kukaa ndani ya Yesu kunamaanisha kufanya kile anachotuomba, kama mwitikio Kwake. “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito” (1 Yohana 5:3).
Ukifikiria juu ya hilo, kukaa ndani ya Yesu ni mojawapo ya dawa za hali yetu ya Laodikia (Ufu. 3:20, Yn. 15:4). Ni siri kuu ya maisha yaliyotimizwa na yenye maana duniani na hadi umilele, lakini kwa njia fulani tunasahau kwa urahisi ushauri wa Yesu. Hatimaye, Yesu anamwambia kila mmoja wetu, “ ‘Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu’ ” (Yohana 15:9), Upendo wa Yesu ndiyo kamba yenye nguvu zaidi inayotuvuta Kwake, na tunapojua upendo huo, tutachochewa sana kuitikia kwa upendo kwa Mungu na kwa wengine.