HomeResourcesSabbath School quarterly

Mahali

27/04/2026

Ingawa huu ni mstari mmoja tu, tunaweza kujifunza mengi sana kutokana na mfano wa Yesu. Muda mrefu kabla ya jua halijachomoza, aliondoka (alijiondoa katika mkukumkuku wa maisha ya kila siku) na kuwa mahali pa upweke pa utulivu ili aweze kuwa pamoja na Baba yake. Je, unaweza kuwazia mazingira haya—Yesu, akiwa ameketi kando ya Bahari ya Galilaya au kando ya kilima, akiomba na kuzungumza na Baba Yake kabla ulimwengu unaomzunguka haujaamka? Ingawa mstari huu unaelezea jinsi Yesu alivyojitoa kwa moyo katika maombi, tunaona wazi kwamba hili lilikuwa suala la kipaumbele Kwake. Bila shaka wakati huu ndio uliompatia nguvu za kukabiliana na yote aliyovumilia. Ikiwa Yesu alihitaji hili ili kuianza kila siku, je, sisi tutafanya zaidi kiasi gani?

Mungu anatuambia, “ 'Nitafuteni uso Wangu,' ” na anatumai jibu letu litakuwa “ 'Bwana, uso wako nitautafuta.’ ” (Zab. 27:8).

Je, una mahali unapoweza kwenda kila asubuhi ili kuwa na Mungu? Labda unaweza kupata kiti karibu na dirisha, mahali penye utulivu nje, au hata meza ya jikoni, ambapo unaweza kuja kila siku kuketi miguuni pa Yesu ili kujifunza toka katika Neno la Mungu. Kuketi miguuni pa Yesu ndipo mahali bora zaidi pa kuwepo (Luka 10:39-42). Kwa kutengeneza mazoea ya kila siku ya kwenda mahali fulani ili kuwa na muda na Mungu, utakuwa na uwezekano mkubwa wa kurudi hapo kila siku. Usivunjike moyo utakaposhindwa kuwa pale siku moja moja, kwa sababu dharura hutokea, na huenda usiweze kutumia muda na Mungu. Lakini jitahidi kutokuruhusu siku, majuma, au miezi mingi kupita bila kutumia wakati pamoja na Mungu. Kumbuka kwamba kuwa na uhusiano wa kudumu na Mungu ni uamuzi wa kila siku, ambao unaweza kuanza tena leo, ukiamua.