HomeResourcesSabbath School quarterly

Imani si Hisia

19/05/2026

Yesu alisema kwamba ikiwa una imani ndogo kama punje ya haradali, utaihamisha milima (Mt. 17:20). Kama umewahi kuiona punje ya haradali, unajua jinsi ilivyo ndogo sana. Lakini, kuwa na imani ndogo kiasi hicho kunaweza kuleta mabadiliko makubwa. Kwa hiyo, lazima imani ni ya muhimu sana na pia lazima ina nguvu kubwa na thabiti kiasi cha kufanya kitu asichoweza kufanya binadamu. Hata hivyo, kama ambavyo punje ya haradali inaweza kukua na kuwa mti mkubwa (Mt. 13:31, 32), imani yetu inapaswa kukua na wala si kudumaa.

Kwa kweli, kwanza kabisa, tunahitaji kiasi fulani cha imani ili kuweza kuwa na uhusiano na Mungu.

Kwanza imetupasa kuelewa kuwa imani sio kitu yakinifu; ni mwitiko wa mwanadamu kutokana na kushawishiwa na Roho Mtakatifu. Mungu ni mwanzilishi mwema, ambaye kupitia kwa Roho Mtakatifu, anatuvuta Kwake tunapomruhusu kufanya hivyo (Yer. 31:3). Tunaokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo ni mwitiko kwa neema ya Mungu tuliyopewa kupitia kwa kifo cha Yesu. Tunaokolewa kwa sababu tunamwamini Mungu kama matokeo ya neema Yake. Hiki ndicho kiini cha kuwa na uhusiano Naye.

Pili, imetupasa kukumbuka kuwa imani si hisia. “wengi hawaitumii imani ile ambayo ni haki na wajibu wao kutumia, mara nyingi wakingojea hisia ile ambayo imani peke yake inaweza kuileta: Hisia si imani; haya mawili ni tofauti, Imani ni ajili yetu kutumia, lakini hisia za furaha na baraka ni za Mungu kutoa.”—Ellen G. White. Maandiko ya Awali, uk. 106.

Watu wengine wanaweza kujisikia kana kwamba hawana imani kwa vile hawajihisi kuwa karibu na Mungu au hawako kama walivyopaswa kuwa kama Wakristo. Lakini imani inahusu kumwamini na kumtumaini Mungu, sio tu katika nyakati njema bali katika giza, au katika dhoruba au hata wakati ambapo huwezi kuelewa kikamilifu kinachofanyika hasa katika maisha yako.

Hisia haipaswi kutawala uzoefu wetu wa kidini au uhusiano wetu na Mungu. Ni hasa wakati tunapodhani tuko mbali na Mungu: ndipo tunapohitaji kutumia imani na kumwita (kama alivyofanya yule baba katika Marko 9:24).