HomeResourcesSabbath School quarterly
Jifunze zaidi
22/05/2026
Tunahesabiwa haki (kusamehewa na kusawazishwa mahusiano yetu na Mungu) kwa imani (Rum. 5:1). Baada ya hapo pia tunatakaswa (kupewa uwezo wa kuwa kama Yesu) kwa imani (Mdo. 26:18). Tunapomkaribisha Yesu maishani mwetu pia tunakuwa watoto wa Mungu kwa imani (Yn. 1:12). Tunaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu (Gal. 2:20).
Hakuna kinachoonekana kuwa dhaifu zaidi, lakini kwa kweli kisichoshindika, kuliko roho inayojiona kutokufaa kabisa na kutegemea kikamilifu katika ustahili wa Mwokozi. Kwa maombi, kwa kujifunza Neno Lake, kwa imani katika kuwepo Kwake kwa daima, udhaifu wa wanadamu unaweza kushikamana na Kristo aliye hai, Naye atawashika kwa mkono ambao kamwe hautawaachilia. —Ellen G. White, The Ministry of Healing, uk. 182.
Imani yao inapaswa iimarishwe kwa maombi ya bidii na kufunga, na unyenyekevu wa moyo. Ni lazima waondokane na ubinafsi kabisa, na kujazwa na Roho na uweza wa Mungu. Maombi ya dhati yenye kuvumilia kwa Mungu kwa Imani—imani inayoongoza katika kumtegemea Mungu kabisa, na kujitoa kikamilifu katika kazi yake peke yake ndiyo yanaweza kumletea mtu msaada wa Roho Mtakatifu katika mapambano dhidi ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.—Ellen G. White, Tumaini la Vizazi Vyote, Sehemu ya pili, uk.39.
Masawali ya Kujadili
Muhtasari: Mungu humpatia kila mtu kipimo cha imani kama msingi wa uhusiano Naye. Kama Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu, Yesu ni kielelezo cha nguvu ya imani kwetu sote. Imani yetu inapokuwa ndogo, tunapokuja kwa maombi na maombolezo tukiwa na moyo uliojisalimishwa, Mungu atatenda miujiza katika maisha yetu (taz, Yer. 31:2-4, 9, 11,12). Atatuongoza katika njia Zake zilizonyoka ili tusijikwae tena, nasi tutakuwa na amani. Yesu ndiye kielelezo kikamilifu katika mambo yote, na kuwa na imani Yake utatuhusianisha na watu Wake katika nyakati za mwisho.