HomeResourcesSabbath School quarterly

Imani ya Yesu.

21/05/2026

Kadiri ulimwengu huu unavyokaribia mwisho wake, sehemu ya ujumbe wa malaika watatu inaelezea watu wa Mungu kuwa wanashika amri za Mungu na wana imani ya Yesu.

Kama ukijifunza jinsi ambavyo Waadventista wa Sabato wameelewa kuhesabiwa haki kwa imani, utaona kwamba katika miaka ya 1890, uelewa wa imani ya Yesu na ujumbe wa malaika watatu vilihimizwa sana kanisani. Hadi kufikia wakati huo, kanisa lilikuwa limeweka mkazo mkubwa katika sheria na kulihitajika mkazo zaidi wa injili. Ellen G. White inaieleza vyema kwa kifupi: Amri za Mungu zimetangazwa lakini imani ya Yesu haijatangazwa na Waadventista wa Sabato kama yenye umuhimu sawa, sheria na injili vikienda bega kwa bega. —Selected Messages, book 3, uk. 172.

Ingawa Waebrania 11 inaorodhesha wanaume na wanawake waliokuwa hodari wa imani, hakuna ambaye amewahi kuwa na imani inayoweza kulinganishwa na ile ya Yesu.

Tunapokuwa na imani ya Yesu, hii inamaanisha kuwa si kwamba tu kwa utii Kwake na kwa Neno Lake tutaiga imani aliyokuwa nayo kwa Mungu, lakini pia kwamba tutakuwa na uzoefu hai wa kila siku wa kuishi na Yesu. Ni kujua na kutenda katika msingi wa kwamba bila kumfanya Yesu kiini cha maisha yetu ya kila siku, hatuwezi kuwa na uhusiano unaookoa na Mungu.

Kuwa na imani ya Yesu kunamaanisha kumruhusu Yesu kukaa ndani yetu, na hivyo kuwa na imani Yake ndani ya mioyo yetu, kwa maana Yesu ndiye msingi wa kweli wa imani yetu. Nyakati zingine imani yetu yaweza kuwa dhaifu na nyonge. Lakini Yesu anastahili (Ufu. 5:9), na imani yake inaweza kudhihirishwa katika uzoefu wetu wenyewe, na kuhesabiwa kwetu, kwa karama Yake ya neema kwa wote waaminio.