HomeResourcesSabbath School quarterly
Bibi Harusi
23/06/2026
Akiwa uhamishoni kwenye kisiwa cha Patmos, mwanafunzi Yohana alioneshwa njozi ya jinsi itakavyokuwa tutakapounganishwa na Mungu milele.
Bibi harusi huwa ni mrembo, na kwenye siku yake ya harusi, kila mmoja anataka amwone. Siku ya harusi ni wakati muhimu wa maisha mapya ya pamoja ya bwana na bibi harusi, na hili litakuwa ni kweli pia kuhusu uhusiano na Mungu wakati arudipo.
Yesu amekuwa akituandalia mahali (Yn. 14:1-3), mahali pazuri ambapo panashangaza sana kuliko tuwezavyo kueleza. Kwa kweli, Lugha ya kibinadamu haitoshi kueleza zawadi ya wenye haki. Itaeleweka tu kwa wale watakaoiona. Hakuna akili yenye kikomo inayoweza kuelewa utukufu wa Paradiso ya Mungu.— Ellen G. White, Pambano Kuu, uk. 556.
Ingawa hatuwezi kuelewa kikamilifu vile mbingu mpya na nchi mpya itakavyokuwa, Mungu anamuonesha Yohana njozi ya mahali hapa ili tupate kuishi tukitazamia kwa shauku ile harusi ambayo itakuwa hivi karibuni. Kwa kweli, tumealikwa kufikiri yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi (Kol. 3:2).
Mungu anaandaa tukio hili kwa uangalifu sana, Naye hataki hii harusi kutujia kama jambo la kushtukiza (Mt. 22:1-14; Mt. 25:1-13)
Ulimwengu ni kusanyiko litakaloshuhudia pale tukio hili litakapokuwa, nasi ni baadhi ya walio muhimu sana kwenye kisa hiki. Tutaungana na bibi harusi, jiji hili ambalo Bwana Yesu atatupeleka kwalo akija mara ya pili. Jambo la kupendeza zaidi ni kwamba, watu wa Mungu (watakatifu) wanaitwa pia bibi harusi (taz. Ufu. 19:7), pengine kwa sababu wamo kwenye mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe (Ufu. 21:2).
Maelezo haya ya Jiji Takatifu yanaonesha kwamba kuna uhusiano wa karibu sana kati ya watu wa Mungu na lile jiji, kwa sababu vyote viwili vinaitwa bibi harusi. Biblia inadhihirisha maelezo ya kina ya Mji Mtakatifu, Yerusalemu Mpya, ambao ni mji mkuu nao huwakilisha ufalme, na unaitwa bibi arusi, mke wa Mwanakondoo.— Ellen G. White, Pambano Kuu, uk. 354.