HomeResourcesSabbath School quarterly

Jifunze zaidi

26/06/2026

Kama hatuipokei dini ya Kristo kwa kujilisha katika Neno la Mungu, hatutastahili kuingia kwenye jiji la Mungu. Kwa kula chakula cha kidunia, kwa kujizoeza kupenda mionjo inayoongoza kupenda mambo ya kidunia, hatungefaa kwa nyua za kimbingu; hatungeweza kuthamini vitu vilivyo safi, mkondo wa kimbingu unaotawala mbinguni. Sauti za malaika na muziki wa vinubi usingeturidhisha. Sayansi ya mbinguni ingekuwa fumbo akilini mwetu. Yatupasa tuwe na njaa na kiu ya haki ya Kristo; inatupasa tufinyangwe na kutengenezwa na nguvu inayobadilisha ya neema Yake, ili tufae kuwa katika jamii ya malaika wa kimbingu....

“Kisha mataifa hayatakuwa na sheria nyingine isipokuwa sheria ya mbinguni. Wote watakuwa ni familia iliyo na furaha, yenye umoja, iliyovishwa mavazi ya sifa na shukrani... Katika mandhari hii, nyota za asubuhi zitaimba pamoja, na wana wa Mungu watapiga kelele za furaha, wakati Mungu na Kristo wataunganika katika kutangaza, Dhambi haitakuwepo tena, wala mauti haitakuwepo tena.

Yapasa tuingie mazoea ya kupazungumzia mbinguni, mbinguni pazuri, Zungumzia yale maisha yatakayodumu kama Mungu anavyoishi, na kisha utasahau majaribu na matatizo yako madogo madogo. Hebu mawazo yavutiwe na Mungu.—Ellen G. White, The Faith I Live By, uk. 363.

Masawali ya Kujadili

Muhtasari: Kadiri tunavyoweka macho yetu Kwenye lengo, hebu tuweze kusema, Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu (Flp. 1:6). Mungu alianzisha uhusiano alio nao nawe, Naye ataukamilisha. Hebu na tukue katika upendo na katika imani tunapoisubiri siku ile, wakati tukidumu kupumzika katika haki ya Kristo, ambayo tunapewa tu kwa imani.