HomeResourcesSabbath School quarterly

Mfuate Mwana - Kondoo

24/06/2026

Je, umepata kuulizwa kile unachokitarajia zaidi katika milele inayokuja? Mtoto anaweza kusema, Kumpakia Chui, kuteleza kwenye shingo ya twiga, au Kupaa kwenda kwenye sayari mbalimbali. Kama ungemwuliza kijana wa umri wa kupevuka, anaweza kusema, kutokabwa na jukumu la kufanya kazi zaidi za nyumbani, au Kuitalii mbingu nikiwa na marafiki zangu bila kuumizwa. Na ikiwa ungewauliza kundi la watu wazima, wanaweza ema, “Kuwa mahali ambapo hapatakuwa na maumivu tena, wala kuteseka, wala kifo,” au “kuunganishwa tena na wapendwa wetu.” Majibu haya yote ni mazuri na ya kweli, na yapo mengi sana ya kutarajia kuona kwenye mbingu mpya na nchi mpya. Milele huwa inawaka moto ndani ye mioyo yetu, na kwa namna iliyo halisi, tunajua kwamba lazima kuna kitu zaidi maishani kuliko wakati huu na sasa.

Kwa kweli baraka kubwa kuliko zote hatimaye itakuwa kumwona Yesu na kumshukuru, kiuhalisia nafsi kwa nafsi, kwa kile ambacho ametufanyia kwenye dunia hii iliyoanguka dhambini. Tutataka kutoa kwa wingi zaidi sifa zetu na ibada kwake Yeye kwa kutuokoa na mauti ya milele, kwa kuteseka kwake binafsi msalabani.

“Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka!” (Ufu 5:12)

Yohana Mbatizaji alimtambulisha Yesu kama Mwana — Kondoo wa Mungu (Yn. 1:36). Wawili kati ya wanafunzi wawili wa Yohana alisikia kauli hii na kumfuata Yesu (Yn. 1:37), na Ufunuo 14:4 inatuambia kuwa inatupasa tufanye vivyo hivyo. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako (Ufu. 14:4). Hata hivyo, ikiwa tunataka tumfuate Yeye hadi mbinguni, sharti tumfuate Yeye kwanza hapa duniani.

Yesu, Mwana — Kondoo, ndiye pia Mchungaji wetu, akiongoza njia zetu kwa namna asivyoweza kufanya mwingine yeyote. Hili linatuthibitishia zaidi tunapopambana tukipitia kwenye nyakati zetu ngumu tunazojikuta, lakini Yesu kamwe hatakoma kutuongoza, hata mbinguni. Ufunuo 7:17 inasema, Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji. Kama watu wake, kondoo wake, tutamfuata Bwana Yesu mbinguni, milele tukitaka kuwa katika kuwepo kwake. Sifa moja inayowabainisha watu wa Mungu ni kwamba Jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao (Ufu. 22:4). Yaani, daima tutakuwa tukimfikira Yeye.