HomeResourcesSabbath School quarterly

Mashujaa wa Maombi

02/05/2026

Somo la Juma Hili

Dan. 2: 20 -23; Dan. 6:10,11; Mdo. 20:36; Mwa. 5:22-24; Kut. 33:15-23; Kut. 32:31,32.

Fungu la Kukariri

“Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote” (#Zab 116:1-2#).

Hebu fikiria ikiwa ungekuwa unazungumza na rafiki yako mpendwa au mwenzi wako kwa nadra. Ndani ya muda mfupi uhusiano huo ungevunjika, na kungekuwa na tatizo. Vivyo hivyo, maombi ni sehemu muhimu ya kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu. Ni tabia muhimu sana ya kiibada, ambayo kila mmoja wetu anaihitaji na anaweza kuiimarisha. Kama hatuombi mara kwa mara na bila kukoma, tutatanga mbali na Bwana muda si muda.

Katika Biblia, tunajifunza juu ya maisha ya watu tofauti walioomba kwa namna tofauti. Tunaweza kurudi nyuma kidogo na kuangazia juu ya namna mazungumzo yao na Mungu, yalivyobadilisha mahusiano yao na Mungu, namna na ni kwa ajili ya nini tunapaswa kuomba na jinsi ambavyo maombi yao yalibadilisha maisha ya wengine. Ni kweli: maisha yetu ya maombi hayabadilishi maisha yetu tu bali na ya wengine.

Kama lilivyo suala la kujifunza Biblia, mada hii ya maombi ina sifa zote mbili ni kubwa na muhimu na pana zaidi ya kile kinachoweza kufundishwa kwa majuma mawili. Juma hili tutajifunza masomo kutoka baadhi wa wale walio katika Biblia ambao walituonesha jinsi maombi yalivyo kiini cha uhusiano imara na Mungu. Hebu tujifunze kutokana na vielelezo vyao.

Jifunze somo la juma hili, ukijiandaa kwa Sabato ya Mei 9