HomeResourcesSabbath School quarterly

Henoko Alitembea na Kuzungumza

05/05/2026

Biblia haielezi mengi kuhusiana na maisha ya Henoko lakini inatuambia kwamba alitembea na Mungu kwa miaka 300 hadi Mungu akamtwaa kwenda mbinguni. Ni jambo zuri kiasi gani kwamba maisha ya mtu yanabainisha na ibada yake ya daima kwa Mungu!

Jambo moja tunalojua ni kwamba Henoko lazima “alidumu katika kusali” (Rum. 12:12) akistahimili, na kuzidi kuimarisha uhusiano wake na Mungu katika imani kupitia katika uzoefu wake wa kila siku. Dunia ilikuwa inazidi kuzama katika uovu katika wakati ambao aliishi, na Henoko akajishughulisha zaidi katika kumtumikia Mungu, lakini asingeweza kulifanikisha hilo pasipo kukaa ndani Yake. “Katikati ya maisha yenye shughuli nyingi, kwa uthabiti Henoko alidumisha mawasiliano yake na Mungu. Kadiri kazi zake zilivyomshinikiza zaidi, ndivyo maombi yake yalivyozidi kuwa yakudumu na makini... Baada ya kubaki miongoni mwa watu, kwa muda fulani, akijishughulisha ili kuwafaidisha kwa mafundisho na kielelezo, alijitenga, ili atumie wakati fulani akiwa peke yake, akiwa na njaa na kiu ya kupata maarifa ya mbinguni ambayo Mungu pekee ndiye anayeweza kuyatoa. Kwa kuwasiliana hivyo na Mungu, Henoko alizidi sana kuakisi sura ya Mungu... hata wasiomcha Mungu waliangalia kwa hofu chapa ya mbingu katika uso wake.” —Ellen G. White, Wazee na Manabii, uk. 85.

Mungu hatuagizi kuishi kama wapweke au watawa, tukijetenga kabisa na ulimwengu kiasi cha kutokuwa na manufaa yoyote duniani. Kama Henoko tunaweza kuwa wenye manufaa na wenye kutambua mahitaji katika maeneo yanayotuzunguka, lakini ni pale tu tutakapotembea na kuzungumza na Mungu, kupitia kwa uhusiano thabiti wa daima ndipo ataweza kuidhihirisha tabia Yake ya ajabu kupitia kwetu.

Tunaweza kuomba wakati wowote mahali popote. Hakuna mahali dunia ambapo Mungu hawezi kutuona au kutusikia (Zab. 139:7-12), daima Anasikia vilio vya mioyo yetu, haidhuru tuwe wapi (soma Maombolezo 3:55-57). Lakini kuna kitu kinachopaswa kusemwa juu ya kuomba kwa sauti badala ya kuomba kimoyomoyo. Tunapoomba kimoyomoyo, mawazo yenu yanaweza kuchepushwa au hata kushindwa kuhitimishwa mlolongo wa fikra zetu, au sentensi zetu. Na linaweza kuwa jambo gumu kwa fikra zetu kumakinika. Bali tunapoomba kwa sauti iwe kwa kunong’ona au kwa sauti yetu ya kawaida, inatukumbusha kwamba Mungu ni halisi, kwamba anasikiliza, na kwamba tuna jambo letu tunalozungumza Naye.