HomeResourcesSabbath School quarterly

Jifunze zaidi

08/05/2026

Hatimaye, tunapaswa kuomba kwa vile tunampenda sana Mungu, na hatuwezi kabisa kumudu kutomweleza kila kitu katika maisha yetu: furaha zetu na “ushindi” maishani, mizigo yetu na hofu zetu, haya zetu na mahitaji yetu ya kila siku “Twaweza kufunga mlango wa kila fikra isiyo safi na mawazo machafu kwa kupandisha roho katika uwepo wa Mungu kupitia maombi ya dhati. Wale ambao mioyo yao iko wazi kupata msaada na mbaraka wa Mungu, watatembea katika hali ya utakatifu kuliko ile iliyoko duniani na watakuwa na mawasiliano ya kudumu na mbingu... Tunahitaji kuwa na mitazamo bainifu kuhusiana na Yesu na ufahamu mkamilifu zaidi kuhusiana na mambo ya umilele.

Mwoneshe Mungu mahitaji yako, furaha yako, uzito wako, mashaka yako na hofu zako. Huwezi kumwudhi Mungu wala kumchosha. Yeye ambaye huhesabu nywele za kichwa chako, hawezi kutojali mahitaji ya watoto wake...

Moyo wake wa upendo huingiwa na huruma, tukiwa na huzuni na hata tukizitaja. Mwambie mambo yote yanayofadhaisha moyo. Hakuna uzito unaomshinda, maana ndiye anayeendeleza dunia zote za mbinguni. Hutawala malimwengu. Hakuna chochote kwake kinachohusu amani yetu ni kidogo Kwake kukiona. Hakuna sura katika uzoefu wetu ambayo ni ya giza kiasi cha Yeye kutoweza kusoma, hakuna mashaka yaliyo magumu Kwake kiasi cha Yeye kushindwa kutatua. Hakuna msiba uwezao kumpata hata mtoto Wake aliye mdogo, wala jambo linalomhangaisha au kumfurahisha, wala hakuna maombi yatokayo moyoni mwa mmojawapo wa watu Wake, bila Baba yetu aliye mbinguni kuyaona yote na kusikia mara moja... Mungu humfikiria na kumwangalia kila mtu kana kwamba hakuna mtu mwingine wa kumshughulikia ila yeye tu ambaye Mwana Wake Mpendwa alikufa kwa ajili yake.” —Ellen G. White, Jipatie Amani Moyoni, uk. 75-76.

Masawali ya Kujadili

Muhtasari: Tunaposoma habari za nguli wa maombi katika Biblia, inaweza kuwa rahisi kudhani kuwa hatuwezi kuwa na uhusiano wa karibu kiasi hicho na Mungu, au Kujitoa kiasi hicho. Lakini tunaweza. Kama Danieli tunaweza kuwa thabiti na waaminifu katika kupiga magoti kila siku, haidhuru kuna upinzani gani. Kama Henoko, tunaweza kuchagua kutembea na kuzungumza na Mungu, tukimgeukia kabla ya kufanya kazi aliyotuita kufanya. Kama Musa, tunaweza kuwaongoza wale walio katika ushawishi wetu, tukifanya maombezi kwa ajili ya familia zetu na wale walio katika jumuiya zetu tunapochagua kukaa chini ya uvuli wa Mwenyezi, Kiongozi na Rafiki yetu.