HomeResourcesSabbath School quarterly
Maombi Yenye Matokeo
09/05/2026
Somo la Juma Hili
Mt. 6:5-8; 1 Fal. 19:1-18;Lk. 11:2-4; Mt. 6:5-15; Dan. 9:4-19; Rum. 8:26,27.
Fungu la Kukariri
“Enyi watu mtumainini siku zote, ifunueni mioyo yenu mbele zake, Mungu ndiye kimbilio letu” (#Zab. 62:8#).
Je, maisha yako ya maombi yakoje? Unaomba mara nyingi kiasi gani? Ni kwa bidii kiasi gani? Ni kwa matarajio kiasi gani? Je, unaomba kila siku, au unaomba wakati wa dharura tu? Je, maombi yako daima ni kwa ajili ya mahitaji ya kitu fulani, au huwa unamsifu Mungu katika maombi yako, pia?
Pia, huwa unaomba asubuhi kabla ya kula na huenda katikati ya siku yako yenye shughuli nyingi? Huenda umekuwa sehemu ya kikundi fulani kinachoomba mara kwa mara au hata umepata uzoefu wa kile kiitwacho kuomba bila kukoma (saa 24). Je, umepata uzoefu wa nguvu na kuwepo kwa Mungu kupitia maombi ambayo yanabadilisha kila kitu katika maisha yako?
Maombi ni muunganiko wa daima kati yetu (matawi) na Yesu (Mzabibu). “Ili tuweze kukua na kustawi, lazima daima tufyonze utomvu na viinilishe kutoka kwa Mzabibu Hai; kwani tukijitenga na Mzabibu tunakosa nguvu” –Ellen G. White, Early Writings, uk. 73. Huu ndio mbaraka wa maombi ya daima. Mungu hutusikia, na daima anajibu kwa wakati Wake na kwa jinsi Yake ifaayo — ingawa si kila wakati itakuwa kama tulivyotarajia.
Juma hili hebu tujifunze waombaji wengine katika Biblia na kuangalia njia halisi za kuimarisha maombi katika maisha yetu ya kila siku.
Jifunze somo la juma hili katika maandalizi kwa ajili ya Sabato, Mei 16.