HomeResourcesSabbath School quarterly

Maombi Yanapoonekana Kutojibiwa

11/05/2026

Hana ni kielelezo cha mwanamke mcha Mungu ambaye aliombea kitu mahususi (1 Sam. 1:10-17). Mwanzoni ilionekana kwamba Mungu hakujibu maombi yake, lakini alidumu kuomba, na Mungu alijibu, katika muda Wake mwafaka na kwa kadiri ya mapenzi Yake. Nyakati zingine kungoja kunaimarisha kutembea kwetu na Mungu, kadiri tunavyojifunza kumtumaini zaidi.

Zaburi 62:8 “Enyi watu mtumainini siku zote, ifunueni mioyo yenu mbele zake, Mungu ndiye kimbilio letu.” Tumaini. Je, tunaamini kwamba kwa kweli anajua kilicho bora, hata wakati tunaposhindwa kuona jibu la mara moja kwa maombi yetu? Je, tunaamini kuwa hatimaye Atajibu katika muda na njia mwafaka Kwake?

Nyakati zingine yawezekana maombi yetu yasijibiwe haraka kama tunavyotaka au kwa namna tunayotumaini kuwa yatajibiwa. Je, Biblia inatupatia ushauri gani juu ya jambo hili?

  • Tafuta mapenzi ya Mungu, na wala si mapenzi yako (Mt. 6:10; 1 Yoh. 5:14, 15).
  • Chunguza msukumo wako wa kuomba (Mit. 16:2, Yak. 4:3).
  • Tafakari iwapo unayodhambi unayoipenda (Zab. 66:18, 1 Pet. 3:12, Mit. 15:29).
  • Kaa ndani ya Mungu na ndani ya Neno Lake (Yohana 15:5).
  • Unapoomba amini (Ebr. 11:6, Yak. 1:6, Mk. 11:24, Mt. 21:22)
  • Chunguza hali ya moyo wako (mnyenyekevu au mwenye kiburi) (Yak. 4:6, 1 Pet. 5:6)
  • Vumilia (1 The. 5:17, 18).
  • Wasamehe wengine (Marko 11:25, 26).
  • Hatimaye, Mungu anaona picha pana na anajua kilichobora kwa ajili yetu (Rum. 8:28; Efe. 3:20, Yer. 29:11-13). Nyakati zingine jibu Lake ni kama Alilompa Paulo “Neema Yangu yakutosha" (2 Kor. 12:9)

Ukweli muhimu unaongoza mwitiko wetu kwa kile kinachoonekana kama maombi yasiyojibiwa ni jinsi tunavyomwelewa Mungu. Kama tunamwona Mungu kama aliye mbali na asiyejali, uhusiano wetu Naye unadorora. Katika nyakati kama hizo, chunguza Biblia ili upate ushahidi wa upendo na uangalizi Wake kwako na uombe kwamba uelewa wako juu Yake uliopotoka utarekebika.