HomeResourcesSabbath School quarterly
Yesu Anatufundisha Jinsi ya Kuomba
12/05/2026
Katika wakati wa Yesu, maombi yaliyokuwa marefu na yaliyoandaliwa kitaalamu kama utendaji — kwa kutumia maneno magumu na mara nyingi yaliyokaririwa yalithaminiwa sana. Yesu hakuona lolote zuri la kuzungumza juu ya maombi haya (taz. Mt. 6:5-8). Aliyafunua kuwa kile walichokuwa: maonesho ya “utakatifu” wa kujifanya.
Wanafunzi walimwona Yesu akiomba, na walijua kuwa maombi yalikuwa sehemu muhimu sana ya maisha Yake (taz. Luka 5:16, Luka 6:12, Luka 9:18, Luka 22:41, Luka 24:30, Marko 1:35, Marko 6:46). Walipomtazama Yesu, waliona tofauti na viongozi wa dini na kutambua kuwa kulikuwa na mengi zaidi kuhusiana na maombi kuliko walichokuwa wakikizingatia. Hivyo, wanafunzi wakamjia Yesu, na kumwomba, “ ‘Bwana, tufundishe sisi kusali’ ” (Luka 11:1).
Yesu alionesha kielelezo kwa wanafunzi Wake (na kwetu) kwamba tunaweza kuomba tu kwa lugha ya kawaida. Alituonesha kuwa maombi yetu yanapaswa kuwa ya dhati na kutoka mioyoni mwetu.
Soma Luka 11:2-4 na Mathayo 6:5-15 na uone vipengele vifuatavyo vya maombi ambavyo Yesu alifundisha:
- Baba yetu uliye mbinguni: Kutambua uhusiano wako binafsi na Baba wa wote.
- Jina Lako litukuzwe: Kutambua utakatifu wa Mungu hutusaidia kuja kwa kicho na heshima.
- Ufalme Wako uje: Kuwa na shauku ya ujio wa Mungu na ukaaji ndani yetu wa Roho Mtakatifu hadi atakapokuja.
- Mapenzi yako yatimizwe hapa dunia kama huko mbinguni: Kujisalimisha na kuomba kwamba mapenzi ya Mungu yatimizwe maishani mwetu, tukitumaini kuwa anajua kilicho bora, badala ya kuomba tu kwa ajili ya kile tutakacho.
- Utupe leo riziki zetu: Kuomba kwa ajili ya kile tunachohitaji ili kuishi, kwa aina zote mbili yaani kimwili (chakula na maji) na kiroho (Yesu na Neno Lake lililo hai).
- Utusamehe deni zetu kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu: kutubu, kutafuta msamaha, na kukumbuka kuwa huru kuwasamehe wale ambao wametuumiza kama anavyotusamehe Mungu.
- Usitutie majaribuni bali utuokoe na yule mwovu: Kuomba kwa ajili ya ulinzi na kimbilio dhidi ya uovu katika ulimwengu huu. (Zaburi 91)
- Kwa kuwa ufalme ni Wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina: Kutambua kuwa vile tulivyo, vile tulivyo navyo, na vyote tufanyavyo ni vya Mungu. Ni Yeye pekee astahiliye utukufu na sifa zetu (1 Nya. 29:11).