HomeResourcesSabbath School quarterly
Dhambi, Injili na Sheria
23/05/2026
Somo la Juma Hili
Waamuzi 14; Marko 9:42-48; Rum. 3:20, Mt. 5:17,18; Rum. 3:28; Mt. 7:24-2.
Fungu la Kukariri
“Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha. Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako” (#Zab. 119:93-94#).
Bila shaka, dhambi ni kizuizi kikuu cha uhusiano wa karibu na Mungu. Si kwamba tu dhambi inatutenganisha na Mungu kwa sasa (Isa. 59:2), bali pia inadanganya, inaumiza, inateketeza, na hatimaye inatuangamiza. Vita yetu dhidi ya dhambi na ubinafsi ni vita kubwa kabisa, ambayo tutapata kukabiliana nayo, ikiwa na matokeo makubwa, yaani ya milele.
Wengine huipuuzia dhambi kama tu sehemu ya kawaida ya maisha. Hata hivyo, ni jambo la asili ya kibinadamu kuendekeza anasa. Je, tunaihafifisha dhambi kwa sababu jamii imeridhika nayo? Tunaweza kuongea kwa tahadhali kubwa juu ya mada ya dhambi, kwa kuogopa kwamba tutamkwaza mtu fulani ikiwa tutaiita dhambi kwa jina lake, lakini mwisho wa yote, kadirl tunavyochagua kuishi nayo bila kukwazana, ndivyo tutakavyozidi kuteleza kwenda mbali na uhusiano bora na Mungu.
Ndio, kila mtu ametenda dhambi, fikra, misukumo, matendo na maneno yetu yanawaumiza wengine, sisi pamoja na Mungu. Mwishowe dhambi inaharibu uhusiano wetu na Mungu, lakini Mungu amejidhihirisha Mwenyewe kwetu kupitia kwa ufahamu wa sheria ambayo huifunua dhambi maishani mwetu. Juma hili hebu tuchungue sababu ya Mungu kutupatia sheria Yake na, na pale mtu anapoivunja sheria ya Mungu na matokeo yake akatenda dhambi, ni kitu gani au ni nani anayeweza kusaidia kurejesha mahusiano yake na Mungu.
Jifunze somo la juma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato, Mei 30.