HomeResourcesSabbath School quarterly
Jifunze zaidi
29/05/2026
Hatupaswi kushangazwa kwamba mada ya sheria inaweza kuwa yenye kupotoshwa kiasi hicho na kutoeleweka, hasa kwa vile changamoto ya Shetani dhidi ya Mungu ilihusu sheria Yake.
Wengine katika siku za Yesu walidhani kuwa alikuwa amekuja kuibatilisha sheria, lakini hilo lilikuwa limeenda mbali kupitiliza kutoka katika kweli. Yesu aliangaza nuru juu ya sheria na tabia ya Mungu ya kupendeza, Naye alikuja kuitimiza sheria (Mt. 5:17,18) kutuonesha vile Mungu alivyo.
“Ni pale tu heshima kwa Neno takatifu la Mungu ingetunzwa mioyoni mwa watu, wangeweza kutumaini kutimiza kusudi la Mungu. Ni kwa kuzingatia tu sheria ya Mungu ndiko kulikowapa Israeli nguvu wakati wa utawala wa Daudi na miaka ya awali ya utawala wa Sulemani; ilikuwa kwa njia ya imani kwa neno hai ndipo matengenezo yaliwezekana kufanyika katika siku za Eliya na Yosia. Na ilikuwa kwa Maandiko hayohayo ya ukweli, urithi tele wa Israeli, ambayo Yeremia alitumia katika juhudi zake za kufanya matengenezo.”—Ellen G. White, Manabii na Wafalme, Sehemu ya Pili, uk. 88.
Masawali ya Kujadili
Muhtasari: Maisha yetu yameathiriwa na dhambi, ambayo inatutenga na Mungu. Hata hivyo, Mungu anatualika kumjua na kumpenda kwa mioyo, akili, roho na nguvu zetu zote. Tunapofanya hivyo, kiasilia tutakuwa na upendo zaidi kwa wengine. Upendo huo kwa Mungu na kwa wengine unaelezwa katika sheria ya Mungu, ambayo ilitolewa ili kulinda na kuhifadhi uhusiano wetu Naye pamoja na wale wanaotuzunguka. Sheria ya Mungu ni udhihirisho mzuri sana wa tabia Yake, na mara tunapoielewa sheria Yake, uhusiano wetu Naye unaimarika.