HomeResourcesSabbath School quarterly
Ngome Imara katika Uhusiano Wangu na Mungu
25/05/2026
Kuna jumbe nyingi katika Biblia zinazozungumzia uhusiano wetu na Mungu na vikwazo vinavyotuzuia kukua katika Kristo. Yatafakari maneno haya kutoka kwa Paulo na Yesu:
“Basi wewe utoapo sadaka, usipige pande mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu” (Mt. 6:2). ‘Acha kumweleza kila mtu jinsi ulivyo mwema. Kuwa mnyenyekevu kama Yesu alivyokuwa mnyenyekevu.
“ ‘lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako Kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanumu’” (Mt. 5:28-29). Fanya chochote kile kuondoa tamaa kutoka moyoni mwako, kwa kuwa hiki ni kizuizi kwa uhusiano wako na Mungu. “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa’ (Mt. 7:1-2). Acha kuwa mkosoaji na mwenye kuwahukumu wengine. Mungu ndiye Mhukumu kwa hiyo mwachie kazi Yake (1 Kor. 4:5).
“lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanao walaani, watendeeni waombeeni mema wale wanaowachukia, na waombeeni wale wanaowatumia kwa uovu na wale wanaowaudhi” (Mt. 5:44 tafsiri kutoka NKJV). Acha kuwachukia adui zako. Unapojisikia vibaya dhidi ya wale wanaokutendea vibaya, mara ile ile inaweka kikwazo Katika uhusiano wako na Mungu. Badala yake anza kuwaombea adui zako nawe utaona jinsi hili linavyobadilisha sio tu matembezi yako na Mungu bali pia uhusiano wako na wengine.
“Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira bila sababu atakuwa katika hatari ya kuhukumiwa” (Mt. 5:22 tafsiri ya kutoka NKJV). Huenda umekuwa ukihalalisha kwa nini unawakoromea wale walio karibu nawe. Je, hasira yako inaathirije uhusiano wako na Mungu, bila kutaja wale unaowakasirikia? Haya ni baadhi ya maeneo yanayotusababisha kujikwaa.
Yesu alionya juu ya kile tupaswacho kufanya wakati mikono, miguu na macho yetu vinapotusababisha kutenda dhambi. Je, Yesu alikuwa anatuonya juu ya nini? Soma Marko 9:42-48