HomeResourcesSabbath School quarterly
Sheria na Injili
27/05/2026
Yesu Mwenyewe alieleza kwa mkazo mkubwa na kwa maneno machache kile Kilichokuwa uhusiano Wake na Sheria.
Kama ambavyo mipaka ambayo wazazi huwawekea watoto wao huonesha kile wanachokithamini, sheria ya Mungu hutuambia juu ya tabia Yake na kile kilicho muhimu Kwake. Mungu alitupatia sheria Yake kulinda uhusiano wetu Naye, na sisi kwa sisi, akijua kuwa sheria Yake ingeongoza kila nyanja ya maisha yetu kadiri tunavyokuwa katika Yeye. Hata hivyo, ni nani ambaye hajawahi kupatwa matokeo ya kutisha ya kile ambacho dhambi, uvunjaji wa sheria, imesababisha kwa kila mmoja wetu?
Upendo kwa Yesu upo katika kiini cha sheria. Yesu alisema, “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” (Yohana 14:15). Tunapompenda Yesu kwa dhati, kiasili tutasukumwa kushika sheria Yake. Tutakapoiona sheria Yake vyema, tutajisikia kusukumwa kumpenda Yesu zaidi. Na hata, cha muhimu zaidi, daima ikidumisha mbele yetu mwonekano wa msalaba na kifo Mbadala cha Kristo kwa ajili yetu ni njia bora kabisa ya kukuza upendo wetu kwa Mungu.
Ndiyo maana injili inaenda bega kwa bega na sheria. Yaani, haidhuru tuamini kiasi gani katika sheria na katika umuhimu wa kuishika, imetupasa kukumbuka kwamba kwa suala la kusimama kwetu kisheria mbele za Mungu, kazi ya sheria ni kuhukumu tu. Kamwe sheria haisemehi kamwe hahesabii haki na kamwe haipatanishi. Kinyume chake, inaonesha kwa nini tunahitaji kusamehewa, kwa nini tunahitaji kuhesabiwa haki na kwa nini tunahitaji kupatanishwa. Ndiyo maana sambamba na sheria — yaani msingi wa uelewa wetu wa sheria — ni injili, kifo cha Kristo kwa niaba yetu, ambacho kinatufanyia kile ambacho sheria haiwezi kufanya kamwe: kutuhesabia haki mbele za Mungu.