HomeResourcesSabbath School quarterly

Kiburi Dhidi ya Unyenyekevu

11/04/2026

Somo la Juma Hili

Yohana 2:15-17; Luka 18:9-14; 1 Yoh. 1:9; Ebr. 11:24-26; Luka 22:24-27, Flp. 2:3-8.

Fungu la Kukariri

“Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa” (#Luka 14:11#).

Sisi sote tumepata kujua watu wanaopenda kujiinua nafsi, wale wanaodhani kwamba kamwe hawakosei. Au pengine unamfahamu mtu ambaye daima anataka kuendesha mambo yote, ambaye kamwe hayuko tayari kwa ajili ya maelekezo au ukosoaji unaojenga. Au mtu anayeonekana kuwa daima katika mapambano au ambaye ni bingwa wa kudhalilisha wengine. Mara moja, mawazo yetu yanaweza kuwafikiria wengine, lakini kwa kweli swali ni hili: Vipi kuhusu kila mmoja wetu? Kwa kuelekeza kidole kwa wengine na kukana kiburi kilichomo kwenye maisha yetu wenyewe, tunajidanganya wenyewe.

Sisi sote tumewahi kupambana na kiburi (au majivuno). Sote tumekuwa na uzoefu wa nyakati ambazo tumetaka kuonekana, kutenda, au kunena, au kuonekana bora kuliko wale wanaotuzunguka kwa sababu tunaamini ya kwamba sisi tu bora kuliko wao, lau kwa namna fulani. Mtu mmoja aliwahi kusema ya kwamba kiburi huwa kinaibukia kwenye shauku ya kuonesha kwamba maisha yetu yana thamani. Hata hivyo yapasa tuwe tunajua tayari ya Kwamba maisha yetu yana thamani kwa sababu tuliumbwa na Mungu, sisi ni wale ambao tupo kwa ajili ya wale ambao Kristo alikufa kwa ajili yao.

Juma hili tutachunguza mguso ambao kiburi kinaweza kuweka kwenye uhusiano wetu na Mungu pamoja na wengine, na tutatazama kile Biblia inachotufundisha kuhusu unyenyekevu mbele za wengine, na, kwa kweli, mbele za Mungu.

Jifunze somo la juma hili kwa maandalizi ya Sabato ya Aprili 18.