HomeResourcesSabbath School quarterly
Jifunze zaidi
17/04/2026
“Tunapozidi kumkaribia Yesu ndivyo tunavyozidi kuona wazi utakatifu wa tabia yake, na kuzidi kuona wingi wa dhambi zetu na tutashindwa kujikweza. Wale ambao mbingu inawaona watakatifu ndio wa mwisho kujitangaza wema wao.” — Lulu za Uzima, uk. 105.
“Kabla ya kupata heshima kwanza kuna kunyenyekea. Kupata cheo mbele ya wanadamu, mbingu huchagua watendakazi ambao, kama Yohana Mbatizaji, wako katika nafasi duni mbele ya Mungu. Mwanafunzi aliye zaidi kama mtoto, ndiye afaaye zaidi katika kazi ya Mungu. Viumbe wa mbinguni wanaweza kushirikiana na yeye ambaye anajitahidi, kutokujiinua nafsi, bali kuokoa roho....
“Lakini watu wanapojitukuza wenyewe, wakijiona kuwa ni wa muhimu sana kwa ajili ya mafanikio ya mpango mkuu wa Mungu, Bwana husababisha wawekwe kando...
“Haikutosha kuwafundisha wanafunzi wa Kristo namna ya ufalme wa Mungu ulivyo. Jambo kubwa walilohitaji ni badiliko la moyo, ambalo lingewawezesha kuwa katika upatanifu na kanuni za ufalme huo.... Usahili, kujisahau nafsi, na kuwa na upendo kama mtoto mdogo, ndizo sifa ambazo Mbingu inazithamini. Hizi ndizo sifa za ukuu wa kweli...
“Roho ya kweli, yenye moyo wa kutubu ni ya thamani machoni pa Mungu. Mungu huweka muhuri wake mwenyewe kwa watu, si kwa kufuata cheo chao, si kwa kufuata utajiri wao, si kwa kufuata ukuu wao wa akili, bali ni kwa sababu ya umoja wao na Kristo.” — Ellen G. White, Tumaini la Vizazi Vyote, Sehemu ya Pili, uk. 45, 46.
Masawali ya Kujadili
Muhtasari: Kiburi kinaweza kuwa mojawapo ya vizuizi vikuu vya ukuaji katika uhusiano na Mungu. Ikiwa tunajisikia hali ya kujitosheleza nafsi na hatutambui hitaji letu la uhusiano huu, hatutaufuatilia. Tofauti na hilo, Yesu alikuwa Mtu mnyenyekevu zaidi duniani na kielelezo bora zaidi cha jinsi ya kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Mungu.