HomeResourcesSabbath School quarterly
Mtazame Yeye
16/04/2026
Kinyume kabisa na shauku ya wanafunzi ya kuwa bora na imani yao kwamba walikuwa bora kuliko mwingine aliyekuwa karibu nao, tunamwona Yesu-mfano mkuu wa unyenyekevu. Yesu, ambaye alisema, “Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye” (Luka 22:27). Yesu, ambaye kila siku aliwaruzuku wale wenye uhitaji waliomzunguka kwa sababu alijawa na huruma na kuyaona makutano kama kondoo wasio na mchungaji. Alijua kwamba jamii ya wanadamu ilimhitaji Yeye kuliko kitu kingine chochote maishani, ingawa ni wachache waliotambua ukweli huu sahili. Yesu, ambaye aliiachilia mbingu ili afe kwa ajili ya wanadamu ili wapate kuelewa tendo Lake la neema na waitikie mwaliko Wake wa kuwa na uhusiano na Yeye.
Yesu alifanya yote. Alibeba yote. Tunapotulia kiasi cha kutosha kumtazama Yeye — kwa uhalisia kabisa — hatuwezi kujizuia kutambua uchafu wetu, taka zetu, na hitaji letu kubwa la kuwa na Yeye maishani mwetu leo.
Tunapomtazama Yeye, jambo lolote lingine (hasa sisi wenyewe na ukuu wetu wa kusadikika) hufifia hadi kufikia udogo kabisa. Yesu ni nani, kile ambacho amefanya, na jinsi anavyopenda uumbaji wake inakuwa ni jambo muhimu na ambalo ni kiini. Nafsi hakika itatoweka tunapomtazama Yeye. Yesu. Ni jina zuri, lenye nguvu ajabu. Yeye ndiye kielelezo cha unyenyekevu. Mioyo yetu illyo wazi inapojifunza kumhusu, tunapoelewa kile ambacho ametufanyia, na tunaporuhusu maneno Yake ya uzima kupenya katika akili zetu, tunatambua jinsi kweli tulivyo na kiburi na duni. Ikiwa wanafunzi Wake mwenyewe, ambao waliishi na kujifunza kutoka Kwake, walisumbuliwa na kiburi, hatuwezi kujidanganya kuwa sisi ni tofauti. Hatimaye, tunaweza kukua katika uhusiano wetu na Yesu pale tu tunapokuwa wanyenyekevu.