HomeResourcesSabbath School quarterly

Vidole Vilivyobanana vya Kiburi

12/04/2026

Kiburi kilianza na Lusifa, yule kerubi afunikaye, ambaye alikuwa katika utumishi wa karibu zaidi na Mungu. Hatujui kwamba ni lini au ni kwa jinsi gani mawazo hayo ya ubinafsi yaliingia moyoni mwake, bali tunajua kwamba mawazo haya yaliusukumia ulimwengu katika kile tunachokijua kama pambano kuu. Tunaona kwamba Shetani yuko kinyume cha Mungu. (Linganisha Isaya 14:12-14 na Wafilipi 2:5-11.) Matokeo yake, dunia yetu imepambana na matokeo ya dhambi tangu Shetani alipopandikiza mashaka kwenye akili za Adamu na Hawa na kisha akawajaribu kupenda na kutumainia nafsi kuliko Mungu.

Je, kiburi kitapata kuwa chanya wakati wowote? Pengine si kwa namna tunavyokijua katika muktadha huu, ingawa tunaweza kulitumia neno hilo kwa namna chanya, tunapozungumzia mafanikio ya mtu au katika muktadha wa shukrani za dhati sana kwa ajili ya kitu fulani ambacho mtu fulani ametenda (“ninaona fahari sana kwa ajili yako!”). Ni muhimu kuelewa kwamba kutafuta ubora na kutambua na kuthamini vipawa na uwezo ambao Mungu amekupa si lazima kuwa na kiburi. Kulingana na Maandiko, kuna aina sahihi ya kujipenda kulingana na Maandiko (fikiria juu ya amri ya Yesu katika Marko 12:31, ambapo anasema tuwapende wengine kama tunavyojipenda wenyewe), lakini daima huu ni upendo usio na ubinafsi. Watu pia hawana kiburi wanapokuwa na uwepo wa Mungu katika maisha yao na kuwa na mwelekeo wenye kusudi (taz. 1 Tim. 3:1). Watu wanakuwa wenye kiburi pale wanapokuwa hawampi Mungu utukufu kwa kile anachofanya katika maisha yao.

Tunapaswa kuwa waangalifu kukumbuka kwamba mali, uwezo na mafanikio yetu haviamui thamani yetu. Badala yake, thamani yetu inapaswa daima itoke kwa Mungu, kwa sababu kila kitu tulicho nacho, hata kile ambacho hutupatia jaribu la kuwa na majivuno, vinatoka Kwake tu. Hili ni jambo ambalo hatupaswi kusahau kamwe.